Askofu wa Kanisa Katoliki Mbeya amesema kama angekuwa na Mamlaka dhidi
ya Waziri angemchapa makofi Waziri aliyeshindwa kutekeleza kauli ya
kuzuia malori yanayoharibu barabara.
“Yupo
Waziri ambaye alisema malori makubwa yanaharibu barabara hivyo mizigo
yote inatakiwa kusafirishwa kwa Reli lakini mpaka sasa hajatekeleza..
kama ningekuwa na uwezo ningemchapa makofi” alisema Askofu Evarist Chengula.
Pamoja na kwamba Askofu huyo hakutaja jina la Waziri huyo lakini aliyekuwa Waziri wa Uchukuzi, Dk Harrison Mwakyembe
aliwahi kutamka kauli kama hiyo ambapo alipoulizwa kuhusu
kilichokwambisha kauli yake amesema kwamba ile haikuwa kauli yake ila ya
Serikali, hivyo wa kuulizwa kwa sasa ni Waziri husika Wizara hiyo
ambaye ni Samuel Sitta.


Note: Only a member of this blog may post a comment.