Monday, April 6, 2015

Anonymous

Alichosema Gwajima, mambo manne ya UKAWA na Rais JK mafanikio TZ… zote kwenye #PB @CloudsFM

Jumatatu ya April 06, miongoni mwa zile zilizopewa Headlines kwenye Magazeti ya leo, Askofu Gwajima amesema hawezi kuwatupa Lowassa na Dk. Slaa, kwa kuwa ni marafiki zake wa siku nyingi, UKAWA waidai Serikali mambo manne kabla ya uchaguzi, madereva wagoma kurudi shule kwa kuwa hawana mikataba ya ajira wanazofanya, mtoto mlemavu amefungiwa darini miezi minne kukwepa mafuriko, Polisi ajiua kwa kujipiga risasi katika kituo cha Polisi huko Tabora, waasisi wa CCM wamekubali utafiti ulioonyesha Pro. Mark Mwandosya anafaa kugombea Urais 2015. 

Taarifa nyingine Rais Kikwete amesema Serikali ya awamu yake inajivunia mafanikio waliyoyapata tangu aingie madarakani,Waziri Bernard Membe amewataka vijana wasikubali kutumika kwa ajili ya uvunjifu wa amani, zaidi ya wakazi 1665, hawana sehemu za kuishi kutokana na mvua kubwa iliyonyesha mkoa Simiwi, bunduki yapotea katika mazingira ya kutatanisha katika kituo cha Polisi Tabora, Watoto 21, wazaliwa katika mkesha wa Pasaka huko Iringa, wapenzi wakamatwa kwa kuuza tiketi za kwenda peponi huko Uingereza na waumini Shinyanga wakaguliwa kabla ya kuingia kwenye ibada ya mkesha wa Pasaka.
Bonyeza play hapa chini kusikiliza uchambuzi wa story zote za Magazeti ya leo…
-via millardayo

USIPITWE! JIUNGE NASI FACEBOOK

Subscribe to this Blog via Email :

TOA MAONI YAKO HAPA (MATUSI HAYARUHUSIWI)

Note: Only a member of this blog may post a comment.