Jumatatu ya March 30, tayari Magazeti ya leo yapo mtaani, POWERBREAKFAST ya CLOUDS FM hufanya uchambuzi wa story zote kubwa zilizopo kwenye Magazeti ya kila siku. unaweza kuzisikiliza hapa…
Kinyan’ganyiro cha kuwania Urais CCM,
kufanya maamuzi magumu mwezi ujao, Serikali kuwasilisha Bungeni muswada
wa sheria ya makosa ya mtandao ambapo mtu atakae sambaza picha cha ngono
mtandaoni kufungwa miaka 7, Askofu Kardinali Pengo amesema amemsamehe Askofu Gwajima kwa kumkashifu, Jeshi la Polisi Dar, linawashikilia watu 15, kwa tuhuma za kutaka kumtorosha Askofu Gwajima
katika Hospitali ya TMJ, Askari Magereza afukuzwa kazi kwa kosa la
kukutwa na fedha bandia, Waziri wa Ardhi, Nyumba na Maendeleo ya Makazi,
William Lukuvi amesitisha kuanza kwa mradi mpya wa mji wa Kigamboni.
Zitto Kabwe
apewa masharti magumu ACT wazalendo, barabara ya msimbazi kufungwa ili
kupisha ujenzi wa barabara ya mabasi yaendayo kasi, Wabunge wagawanyika
muswada wa mabadiliko ya sheria mbalimbali, Wizara ya Uchukuzi
inatarajia kujenga reli mpya tatu ili kutoa huduma kwa nchi jirani na
Rais wa Zimbabwe, Robert Mugabe ametoa wito kwa vijana wa Afrika kupinga dhana ya ukoloni mamboleo.
Katika uchambuzi huo kulikuwa na mazungumzo ya Askofu Kardinali Pengo ambae amesema amewasamehe wale wote walioeneza hivi karibuni maneno ya kashfa yasiyofaa dhidi yake.
Bonyeza play kusikiliza uchambuzi wote wa Magazeti ya leo March 30.
-source Clouds FM via millardayo

Note: Only a member of this blog may post a comment.