Pedro Aguayo Ramirez aliyejulikana kwa jina la Hijo del Perro Aguayo alifariki baada ya kupigwa teke na Rey Mysterio
Uchunguzi kuhusiana na uwezekano wa kosa la kuua bila kukusudia,
umefunguliwa baada ya mtoto wa mcheza mieleka maarufu wa Mexico kupoteza
maisha baada ya kupigwa wakati wa mechi.
Taarifa kuhusu kuanza kwa uchunguzi huo imetolewa na ofisi ya mashtaka ya jimbo Baja California.
Pedro Aguayo Ramirez, aliyejulikana kwa jina la Hijo del Perro
Aguayo, alianguka na kupoteza fahamu kwenye kamba za ulingoni baada ya
kupigwa teke na mchezaji mieleka wa zamani wa WWE, Oscar Gutierrez,
maarufu kama Rey Mysterio Jr. kwa mujibu wa video ya mechi hiyo.
Pambano hilo liliendelea kwa karibu dakika mbili kabla ya kugundua kuwa Aguayo alikuwa ameumizwa vibaya.
Alipelekwa kwenye hospitali lakini alifariki baadaye, jana Jumapili.
Aguayo, 35, alipigana mieleka kwa miaka 20 na alikuwa mtoto wa Pedro “Perro” Aguayo, ambaye kwa sasa amestaafu.
Aliwahi kushinda mataji mengi ikiwemo ushindi wa uzito wa juu wa
taifa na mengine. Mcheza mieleka huyo alifariki kutokana na kuumia shingo
na mgongo.
Baada ya tukio hilo, Rey Mystereo alitumia Instagram kusikitishwa kwake kwa kuandika:
“I had the privilege to share a ring for the first time with Hijo
del Perro Aguayo in his debut as a professional wrestler and an honor
to be in the ring with this great legend for the last time! You will be
missed, Perro. Just formed a friendship between brothers who opened
years ago and we should not question the designs of God. But in this
occasion I wonder why and I do not understand it … I take you with me
for the rest of my life, rest in peace HijoDelPerro.”

Note: Only a member of this blog may post a comment.