Thursday, March 26, 2015

Anonymous

POMBE YA MBEGE YAZUA TIMBWILI NI MCHANA KWEUPE, AFUNGA BARABARA, USAFIRI UBUNGO WATIBUKA


DEOGRATIUS MONGELA NA CHANDE ABDALLAH 
ULEVI asubuhi! Pombe maarufu kwa jina la Mbege hivi karibuni ilizua timbwili la aina yake baada ya mama anayeuza kilevi hicho maarufu mama Manka kulazimika kuwajia juu wateja wake wawili ambao ni makondakta wa mabasi yaendayo mikoani katika stendi kuu ya Ubungo jijini Dar es Salaam. 

Shuhuda wa tukio hilo lililojaza watu alisema lilitokea asubuhi ya Machi 20, mwaka huu chini ya daraja jipya lililojengwa na Kampuni ya Strabag lililopo katika mradi wa barabara ya mabasi yaendayo kasi ambapo makonda hao walikuwa miongoni mwa wateja waliokuwa wakinywa kinywaji hicho kinachouzwa kiasi cha shilingi elfu moja kwa kikombe. 

Ghafla, zogo liliibuka baada ya mama Manka kubaini kuwa vijana wawili wanaofanya kazi kwenye mabasi yaendayo Kanda ya Nyanda za Juu Kusini, walikuwa wanataka kuondoka bila kumlipa fedha zake, jambo lililomfanya kuja juu, kabla ya kutulizwa na wateja wengine wakimtaka apunguze munkari ili kuzuia ‘inzi’ waliokuwa wanaanza kujaa. 

Kufuatia jazba alizokuwanazo mama huyo, aliziba barabara kwa muda jambo lililosababisha kutibua usafiri Ubungo Stand.Ingawa baada ya kushtukiwa makonda hao walidai kuwa walishalipa fedha hizo, lakini baada ya mama huyo kuwaganda na kudai kutolipwa, hatimaye walilipa na kuondoka kimya kimya. 

Hata hivyo, kitendo cha makonda hao wa basi kunywa ulabu mida hiyo kuliwafanya baadhi ya watu kuunganisha tabia hiyo na ajali za mara kwa mara zinazotokea.“Yaani hii inaonesha kiasi gani hawa makonda na madereva walivyo. Wanalewa weee, halafu wanakosa umakini barabarani na kusababisha ajali kizembe,” alisema mama mmoja aliyeficha jina lake kuogopa lawama.

USIPITWE! JIUNGE NASI FACEBOOK

Subscribe to this Blog via Email :

TOA MAONI YAKO HAPA (MATUSI HAYARUHUSIWI)

Note: Only a member of this blog may post a comment.