Zari the Bosslady ambaye anatarajia kuwa mama wa mtoto wa nne ambaye
baba yake ni Diamond Platnumz, ameweka picha ambayo imezua hisia kuwa ni
ishara ya jinsia ya mtoto wanayetarajia kumpata.
Kupitia akaunti yake ya Instagram Zari ameshare picha ya kivazi cha
mtoto wa kike kilichoandikwa ‘Princess’ katika kipindi hiki ambacho ni
mjamzito ikiwa ni ishara kwamba tayari wameshafahamu jinsia ya mtoto
wanayetarajia kumpata na staa wa ‘Ntampata Wapi’ Diamond Platnumz.
Hakuandika chochote kwenye picha hii ya Instagram zaidi ya kuweka emoji ya kisura chenye makopa kwenye macho.
Lakini kupitia Facebook Zari amethibitisha kuwa anatarajia mtoto wa kike kwa kuandika:
“Good morning fam while another is sharing thier news of hooking
up with a stripper/PornStar/Hooker as their latest catch. Allow me to
share my amazing news…..here it is”
Zari ni mama wa watoto watatu wa kiume aliowapata na mume wake wa zamani Ivan Ssemwanga.

Note: Only a member of this blog may post a comment.