Agnes Gerald” Masogange “
Na Mayasa Mariwata,
RISASI mchanganyiko
DAR ES SALAAM: Video Queen nyota, Agnes Gerald maarufu kama Masogange anadaiwa kutaka kumharibu muuza nyago chipukizi Asha Salum ‘Kidoa’ baada ya wadau kutilia shaka ukaribu wao.
DAR ES SALAAM: Video Queen nyota, Agnes Gerald maarufu kama Masogange anadaiwa kutaka kumharibu muuza nyago chipukizi Asha Salum ‘Kidoa’ baada ya wadau kutilia shaka ukaribu wao.
Kwa mujibu wa chanzo cha uhakika, katika siku za hivi karibuni mabinti
hao wamekuwa na urafiki wa karibu, wakichati mambo mengi kwenye mtandao
wa kijamii wa Instagram, kitu kinachoonesha huenda ushosti wao ukafika
mbali zaidi ya hapo.
“Si unajua Masogange ana zile dili zake za kwenda mara kwa mara Sauz
huku ikiwa haijulikani hasa anafuata nini? Na si unakumbuka ule msala
wake wa kukamatwa na madawa ya kulevya? Sasa wadau wanahofu asije naye
akaingizwa kwenye mchongo,” kilisema chanzo hicho.
Asha Salum ‘Kidoa’
Katika kuweka sawa madai hayo, gazeti hili liliwasiliana na Kidoa
ambaye alifunguka; “Mimi ni mtu mzima na akili zangu timamu, siyo kila
rafiki utakayekuwa naye basi lazima uige tabia zake, halafu Masogange
siyo rafiki yangu kihivyo, kawaida tu!”
Kwa upande wake, Masogange alipotafutwa na kuulizwa kuhusu madai hayo, alijibu kwa kifupi; “Ulishawahi kuniona nikienda naye Sauz, au ulishawahi kuniona naye kwenye ndege, kifupi mimi sinaga rafiki.”
Kwa upande wake, Masogange alipotafutwa na kuulizwa kuhusu madai hayo, alijibu kwa kifupi; “Ulishawahi kuniona nikienda naye Sauz, au ulishawahi kuniona naye kwenye ndege, kifupi mimi sinaga rafiki.”

Note: Only a member of this blog may post a comment.