Wednesday, March 11, 2015

Anonymous

NYUMA YA PAZIA: DUDE, ESTER KIAMA WA BONGO MUVI MMMH...!

Hamida Hassan/mchanganyiko  
UKARIBU wa mastaa wa filamu za Kibongo, Kulwa Kikumba maarufu kama Dude na msanii mwenzake Ester Kiama unaonyesha kama kuna kitu kati yao baada ya kuonekana kuwa karibu kwa muda mwingi kiasi kinachotia shaka!
Staa wa filamu za Kibongo, Kulwa Kikumba maarufu kama Dude.
Chanzo kilicho karibu na wawili hao kimesema mara kwa mara wanaonekana kuwa karibu kila wanapokwenda na kuonyesha dalili zote za kimahaba, lakini wenyewe wanadai ni washkaji walio kazini.
Gazeti hili lilibahatika kuwafuma wakiwa pamoja na walipoulizwa juu ya tuhuma za kujihusisha kimapenzi, kila mmoja alimtupia msalaba wa kujibu mwenzake.  “Mh, jibu wewe, mimi najua Dude ni kaka yangu na ni mfanyakazi mwenzangu”, alisema Ester.

USIPITWE! JIUNGE NASI FACEBOOK

Subscribe to this Blog via Email :

TOA MAONI YAKO HAPA (MATUSI HAYARUHUSIWI)

Note: Only a member of this blog may post a comment.