Askari akiwa ndani ya duka la vinywaji akifanya mahojiano na wahusika.
VITENDO vya ujambazi vinazidi kushika kasi kwenye
jiji la Dar es Salaam, ambapo tukio lingine limetokea leo mishale ya saa
kumi jioni maeneo ya Mikocheni Kwa-Mwalimu Nyerere baada ya watu wanne
kutinga eneo hilo wakiwa na pikipiki na kumpora mlinzi silaha aina ya
Shot Gun aliyekuwa akilinda kwenye ATM ya CRDB. Majambazi hao waliitumia bunduki hiyo kwa kuvamia duka la vinywaji lililokuwa jirani na kuiba kiasi kikubwa cha pesa japo hakikuweza kufahamika kwa wakati huo.
Mtandao huu ulifanya juhudi za kumpata Kamanda wa Polisi Mkoa wa Polisi Kinondoni, Camillus Wambura ili kupata undani wa tukio hilo na kiasi cha fedha kilichoibiwa ila simu yake ya mkononi ilipokelewa na msaidizi wake aliyedai kuwa kamanda alikuwa katika kikao.
(HABARI/PICHA: MAYASA MARIWATA NA SHANI RAMADHANI/GPL)

Note: Only a member of this blog may post a comment.