Nyumba aliyokuwa akiishi marehemu Maalim Gulumo.
Mayasa Mariwata/ijumaawikienda MKE
wa aliyekuwa mwimbaji dansi Bongo, marehemu Muhidin Maalim Gurumo
(Pichani), Pili Nassor amesema anamshukuru Mungu baada ya watoto wa
mumewe kukaa na kukubaliana kutoiuza nyumba aliyokuwa akiishi na mumewe
huyo iliyopo Tabata jijini Dar.Hivi karibuni, kuliibuka mtafaruku mzito kati ya mjane huyo na watoto wa mare-hemu Gurumo waliokuwa wakishi-nikiza nyumba hiyo iuzwe ili wagawane fedha lakini mjane huyo akasimama kidete hadi wakamwelewa ambapo wamemaliza tofauti zao na sasa wanaishi vizuri.
“Namshukuru Mungu, sasa hivi nina maelewano mazuri na watoto na suala la kuuza nyumba kwa sasa halipo tena, nina mpango wa kuanzisha biashara zitakazoweza kunisaidia kukidhi mahitaji yangu mbali na lile gari alilotoa Diamond (Nasibu Abdul) ambalo tumelifanya teksi,” alisema Pili.


Note: Only a member of this blog may post a comment.