Taarifa kutoka eneo la tukio zinasema kuwa mvua kubwa iliyoambatana na upepo,mawe imenyesha usiku wa kuamkia leo na kuangusha nyumba na miti katika eneo hilo.
Hali hiyo inadaiwa kuleta majanga zaidi kutoka na nyumba zilizojengwa kwa udongo kuharibiwa vibaya na mvua hiyo kubwa.
Habari kutoka eneo la tukio zinasema hali siyo shwari kwani nyumba nyingi zimeharibiwa vibaya,miti imeanguka na sasa miili ya marehemu na majeruhi inakimbizwa katika hospitali ya Kahama.
Kandili Yetu imeambiwa kuwa hadi sasa mvua bado inaendelea kunyesha ingawa siyo kubwa kama ile ya usiku na viongozi mbalimbali wa serikali kutoka wilayani Kahama wamefika eneo la tukio.
Kandili Yetu inafuatilia tukio hili,tutakuletea taarifa kamili hivi punde,endelea kutembelea hapa!
-via Malunde1


Note: Only a member of this blog may post a comment.