Friday, March 20, 2015

Anonymous

LIVE! Mke wa mtu alivyomponza Muhogo Mchungu… #Hekaheka

Muigizaji mkongwe Muhogo Mchungu alikuwa akipiga story kwenye kipindi cha Leo Tena, akizungumzia sanaa amesema anapenda kuigiza kama mtu mwenye maisha ya hali ya chini kuhusu sehemu ambayo huwa anaona ngumu ni kuigiza kama mgonjwa wa akili na kuhusu kuigiza sana kama mtu mwenye nyumba ndogo amesema watu ndio wanampanga acheze hivyo.

Akizungumzia Hekaheka ambayo iliwahi kukutana nayo kuna siku walienda Shinyanga kwenye michezo ya jadi kitaifa akakutana na dada mmoja ambae alitaka kufanya filamu, katika kutumiana ujumbe mume wake akaona akampigia simu na kumtuhumu kutembea na mke wake akamweleza walikuwa wanawasiliana kuhusu filamu waliyotaka watengeneze, jamaa huyo hakumuelewa na kumtishia kumuua ingawa hakuogopa lakini badae alizungumza na mke wake akamwambia yameisha. 

Kuhusu watu ambao anapenda kucheza nao kwenye filamu amesema anaelewana sana na Bi staa kutokana na kuanza wote sanaa, kuhusu kazi alizofanya amesema anapenda sana Tamthilia ya Fukuto na kwa upande wa filamu anapenda sana filamu ya Kigodoro.
Bonyeza play kusikilia Hekaheka yote mtu wangu… -via millardayo

USIPITWE! JIUNGE NASI FACEBOOK

Subscribe to this Blog via Email :

TOA MAONI YAKO HAPA (MATUSI HAYARUHUSIWI)

Note: Only a member of this blog may post a comment.