Friday, March 20, 2015

Anonymous

DUNIA INA MAMBO: Mwanaume kajifanya mwanamke ili afanye kazi Bar, kilichofuatia ni story..

TZA KE JAMAA ALIYEJIFANYA MWANADADA KWENYE BAR AKAMATWA
Ugumu wa maisha unaongeza ubunifu, ubunifu mwingine unakuweka pabaya.. huu wa huyu jamaa sidhani kama tunaweza kuuita ni ubunifu ila jamaa aliamua tu atumie njia hii ili apate tu njia ya kupata mkate wa siku. 

Mmiliki wa Bar ya Siaya, Kenya alimshtukia jinsia ya mmoja ya wahudumu wake wa Bar kwamba jinsia yake sio ya kike.. Akatoa taarifa Polisi kuhusu mhudumu huyo, walipokuja kumpekua jamaa alijitetea kwamba ana jinsia mbili. 

Jamaa huyo anaitwa Michael Obiero alikamatwa baada ya kufanya kazi kwa siku mbili kwenye Bar hiyo akijitambulisha kwa jina la Brenda na pia alikuwa akilala chumba kimoja na wahudumu wengine wa kike. 

Polisi walimlazimisha avue nguo zake ili wamkague, wakaona hakuwa na muonekano wa jinsia ya kike, wanaendelea na upelelezi ili kujua ukweli japo Mkuu wa Polisi Kaunti ya Bondo amesema hata mmiliki wa Bar hiyo huenda akawa na makosa ya kumuajiri jamaa huyo bila kumkagua.

USIPITWE! JIUNGE NASI FACEBOOK

Subscribe to this Blog via Email :

TOA MAONI YAKO HAPA (MATUSI HAYARUHUSIWI)

Note: Only a member of this blog may post a comment.