Friday, March 20, 2015

Anonymous

LIL WAYNE: DRAKE ALINITHIBITISHIA KULALA NA MPENZI WANGU NIKIWA GEREZANI

Lil Wayne (kulia) na Drake.
RAPPA wa nchini Marekani, Lil Wayne katika kitabu chake ambacho kitatoka hivi karibuni, amefunguka kuwa wakati yupo gerezani, mwanamuziki mwenzake aitwaye Drake alimthibitishia kulala na mpenzi wake.
Lil Wayne akiwa stejini na Drake.
Lil ameyafunguka hayo katika muswada wa kitabu chake kipya kitakachotoka hivi karibuni. Lil ameandika kuwa akiwa gerezani katika Kisiwa cha Rikers, Julai 2007 akitumikia kifungo cha miezi nane kwa kumiliki silaha kinyume na sheria, Drake alikiri kulala na mpenzi wake.

Weezy aliongeza kuwa wakati akitumikia kifungo hicho, Drake alimtembelea na kukiri kwa kusema, "Ndiyo, ni kweli. Usilale naye tena kama ulivyokuwa ukifanya awali maana tayari nimefanya naye mapenzi."

Wayne aliandika, "Huu ni upuuzi ambao mwanaume yeyote hasingependa kuusikia hasa akiwa gerezani. Labda, maana Mungu pekee ndiye ajuaye nini ningekifanya kama nisingekuwa gerezani kwa wakati huo."
Wayne ameelezea kwenye muswada huo kuwa, yeye na mpenzi wake walibishana sana, ndiyo maana Drake aliamua kumwambia ukweli kuwa "Usifanye nae mapenzi tena kama awali."
Baadaye mpenzi wake huyo pia alikiri kufanya mapenzi na Drake siku moja kabla ya kukutana na Wayne.
Lil alizidi kufunguka kuwa baada ya kuambiwa taarifa hiyo alijisikia vibaya mno na kuchukulia tukio hilo kuwa baya kuliko mengine yote aliyowahi kukutana nayo maishani.

Lil akizidi kumwaga ubuyu aliongeza kuwa "Kama mwanaume, ni wazi, kitu hicho kiliniuma sana na siyo kwa sababu alikuwa Drake, hata kama angekuwa mwanaume mwingine. Ingeniuma sawa."

USIPITWE! JIUNGE NASI FACEBOOK

Subscribe to this Blog via Email :

TOA MAONI YAKO HAPA (MATUSI HAYARUHUSIWI)

Note: Only a member of this blog may post a comment.