Wednesday, March 4, 2015

Anonymous

LICHA YA MBWEMBWE ZOTE ALIZONAZO, NISHA WA BONGO MUVI ANAHOFIA HII KITU!

GLADNESS MALLYA/mchanganyiko11 
MSANII wa filamu Bongo, Salma Jabu ‘Nisha’ ambaye alitumia muda wake mwingi katika maisha yake ya ujana kwa  kujirusha, amesema sasa yatosha na kwamba huu ni muda muafaka kutengeneza maisha yake ya baadaye.
Msanii wa filamu Bongo, Salma Jabu ‘Nisha’.
Akipiga stori na gazeti hili, Nisha alisema kwa sasa ameamua kuachana na maisha hayo kwa vile umri unakwenda na ni vyema akatumia muda uliobaki kufikiria kuhusu maendeleo yake, hasa yajayo. 

“Naogopa sana kuja kujutia ujana wangu uzeeni, maana unaambiwa fainali uzeeni, kama ni starehe nimeshafanya nyingi sana, sasa hivi nimeamua kuachana nazo maana sioni faida yake,” alisema Nisha.

USIPITWE! JIUNGE NASI FACEBOOK

Subscribe to this Blog via Email :

TOA MAONI YAKO HAPA (MATUSI HAYARUHUSIWI)

Note: Only a member of this blog may post a comment.