Baada ya watu kuhoji ishu ya kampuni ya Kidoti kutengeneza ndala ambazo ni maalum kwa wanawake na kuonekama kama amewasahau wanaume, 255 imemtafuta Jokate
ambae amesema kutakuwa na brand maalum ya wanaume na wataanza kuzipata
muda wowote, akizungumzia kuhusu bei kuwa juu amesema watu wanaochukua
ndio wanapandisha bei kutokana na gharama za kwenda kuzichukua.
Mwanamziki Vee Money wiki hii anategemea kuachia ngoma mpya aliyomshirikisha Rapa kutoka Afrika Kusini KO,
akizungumzia ngoma hiyo amesema ni wimbo unaohusu mapenzi ya dhati
ambao ni maalum kwa watu wote wanaopendana, kuhusu kumshirikisha KO
amesema alikuwa anatamani kufanyanae kazi kwa muda mrefu lakini hakuwa
na uhakika kama atapata ushirikiano lakini aliweza kuzungumza nae na
kufanikiwa kufanya nae kazi.
Muigizaji Wema Sepetu amesema mitandao ya kijamii inanafasi kubwa katika maisha yake hasa katika maswala ya utangazaji na kutolea mfano mtandao wa Instagram
na kusema, umerahisisha kazi kutokana na kutumiwa sana katika
matangazo, yeye ameweza kujua maduka mengi na vitu vingi kupitia mtandao
huo na endapo mtu akitaka apost kazi yake kwenye page yake ni kama dola
elfu moja au elfu mbili lakini inategemea na makubaliano.
-via millardayo

Note: Only a member of this blog may post a comment.