Tuesday, March 31, 2015

Anonymous

CHUMBANI ZAIDI: MUMEO ANAKURIDHISHA MCHEPUKO WA NINI?!

Asalaam alaykhum shoga yangu! Kwa upande wangu nipo vizuri sana kuanzia kiafya pamoja na kiuchumi.
Shoga, kabla sijaanza kukueleza nilichokuandalia leo, napenda kumpa pole mama wa mabinti wawili wakazi wa mkoani Pwani kwa masaibu yaliyowapata ya kubakwa na baba yao mzazi.


Hakika tukio hilo limenihuzunisha sana mbaya zaidi ni pale baadhi ya ndugu wa mumewe wanampomtishia maisha mama huyo kwa kitendo cha kumfikisha mumewe kwenye vyombo vya sheria.Baada ya kusema hayo sasa narejea kwenye mada yangu inayohusiana na wenzetu ambao licha ya kuridhishwa kwa kila kitu na waume zao bado wapo bize na michepuko. 

Shoga, kitendo hicho kinashangaza na kusikitisha kumuona mwanamke ambaye kila anachokihitaji kutoka kwa mumewe anapata lakini anatoka kwenye njia kuu.Ukiacha kutimiziwa mahitaji yote pamoja na kupewa usafiri wa ukweli, mumewe anampa haki yake ya ndoa ipasavyo hadi mtoto wa kike roho inakuwa kwatu lakini bado ‘anamchiti.’ 

Najiuliza wenzetu wanaofanya hivyo sijui wana matatizo gani vichwani mwao, hivi hawajui kama Ukimwi bado upo na unaua mamia ya watu kila siku?Kuna siku nilikuwa nipo katika saluni moja maarufu pande za Kinondoni, Dar naweka sawa nywele zangu, nikamsikia shoga yetu mmoja akiwaambia wenzake jinsi anavyotoka na Kiserengeti boy kwa madai ni ki-handsome. 

Alikuwa akimwambia mwenzake kwamba mumewe anamjali kwa kila kitu hata wakiwa kwenye makasheshe yupo vizuri lakini tatizo eti siku hizi kaanza kuchoka kiasi wakitoka ‘out’ hawaendani ndiyo maana kaamua kuwa na Kiserengeti boy. 

Kwa kuwa nakerwa na tabia hiyo nilimwambia alikuwa akikosea sana na kumweleza madhara yake, akanieleza siku hizi kuwa na dogodogo wa kumlea nje ya ndoa ndiyo fasheni ya mjini.
Aliponieleza hivyo, nilibadili mada kwani nilijua akili itakuja kumkaa sawa siku mumewe atakapobaini anamsaliti. 

Shoga yangu mwenye tabia hiyo, huna sababu ya kuwa na mchepuko hata kama uwezo wa mumeo ni mdogo kwa sababu heshima ya mwanamke ni kutulia kwenye ndoa na kinyume chake ni kuachwa kwa aibu.
Ikiwa mumeo anakabiliwa na tatizo la upungufu wa nguvu za kiume, usitoke nje bali msaidie apate tiba ili mambo yaende sawa. Bye.

USIPITWE! JIUNGE NASI FACEBOOK

Subscribe to this Blog via Email :

TOA MAONI YAKO HAPA (MATUSI HAYARUHUSIWI)

Note: Only a member of this blog may post a comment.