BONDIA
maarufu nchini wa ngumi za kulipwa, Francis Cheka aliyehukumiwa kifungo
cha miaka mitatu jela na kutakiwa kulipa fidia ya Sh. milioni moja kwa
kosa la kumpiga na kumjeruhi meneja wa baa yake amebadilishiwa adhabu ya
kifungo.
Cheka amechiwa na kutoka gerezani na sasa anatakiwa kutumikia kifungo cha nje.
Bondia
Francis Cheka akiongea na wanahabari baada ya kumchakaza Thomas Mashali
tarehe 1 Mei, 2013 katika ukumbi wa PTA jijini Dar Es Salaam.
Cheka amechiwa na kutoka gerezani na sasa anatakiwa kutumikia kifungo cha nje.
(Picha na
Maktaba)
Cheka alihukumiwa na Hakimu wa Mahakama ya Mkoa wa Morogoro, Said
Msuya baada ya kumkuta na hatia ya kumpiga aliyekuwa meneja wa baa yake
iitwayo Vijana Social iliyopo Morogoro Mjini aitwaye Bahati Kabanda
‘Masika’.

Note: Only a member of this blog may post a comment.