Unakumbuka kipindi Jaguar alivyodaiwa kufunga ndoa kimya kimya baada
ya picha zake kusambaa mtandaoni akibadilishana viapo na msichana mrembo
lakini ikaja kubainika kuwa ilikuwa ni video ya wimbo wake One
Centimeter?
Unakumbuka jinsi watu walivyodhani kuwa Ommy Dimpoz amemchukua ex wa
swahiba yake, Diamond, Wema Sepetu baada ya kusambaa picha za utata za
wawili hao lakini kumbe ikaja kubainika kuwa ni Wema ni Wanjera kwenye
video ya Ommy ya wimbo wake mpya?
Na sasa ni zamu ya Akothee, msanii wa Kenya anayefahamika kwa utajiri
wake! Muimbaji huyo amewaacha watu njia panda baada ya kushare picha
akionekana kufunga ndoa ya kifahari mbele ya umati mkubwa wa watu wenye
mchanganyiko wa rangi mbalimbali.
Mashabiki wake kwenye Facebook wanaendelea kumpongeza kwa kuolewa.
“Real friends for life thanks once again for attending my wedding,”
ameandika Akothee. Jionee picha za harusi hiyo pamoja na zingine
anazoonekana muimbaji huyo na mume wake mpya!

Note: Only a member of this blog may post a comment.