10 PICHAZ: MAMIA WAMZIKA ABDUL BONGE KIJIJINI KWAO MKUYUNI, MATOMBO MKOANI MORO
Maziko
ya Mwanzilishi na aliyewahi kuwa Meneja wa Kundi la Tip Top Connection,
Abdul Bonge yakifanyika leo kijijini kwao Mkuyuni, Matombo mkoani
Morogoro.
Mwili wa Abdul Bonge ukiombewa kabla ya maziko leo.
Wanamuziki mbalimbali wakiwemo Shetta, Diamond Platnumz, Profesa J, Quick Racka wakishiriki maziko ya Abdul Bonge.
Mwanamuziki Diamond Platnumz akishiriki swala ya kumuombea marehemu.
Mwili wa Abdul Bonge ukitolewa ndani kupelekwa eneo la kuombewa.
Mdogo
wa marehemu Abdul Bonge ambaye ni Meneja wa Mwanamuziki Diamond
Platnumz, Hamisi Shaban ‘Bab Tale’ akilia wa simanzi juu ya jeneza lenye
mwili wa mdogo wake.
Bab Tale akiwa na majonzi baada ya mwili wa mdogo wake kutolewa nje.
Waombolezaji wakijaribu kumtuliza Bab Tale.
Wanamuziki
Shilole (kushoto), Madee (katikati) wakiwa na Meneja wa TMK Wanaume
Family, Yamoto Band na Diamond, Said Fella wakati wa mazishi ya Abdul
Bonge leo mkoani Morogoro.
Wanamuziki Dully Sykes, Diamond Platnumz na Shetta wakiwa katika mazishi ya Abdul Bonge leo.
HATIMAYE mdau wa muziki nchini ambaye ni Mwanzilishi na aliyewahi
kuwa Meneja wa Kundi la Tip Top Connection, Abdul Shaban Taletale
'Abdul Bonge' amezikwa leo Kijiji cha Mkuyuni kilichopo Matombo mkoani
Morogoro.
Mamia ya waombolezaji wakiwemo wanamuziki Diamond Platnumz, Dully
Sykes, Shetta, Shilole, Dogo Janja, Profesa J, Quick Racka na wengineo
wameshiriki mazishi ya Abdul Bonge.
Abdul Bonge alifariki dunia jioni ya Machi 28 mwaka huu baada ya
kuanguka alipokwenda kusuluhisha ugomvi wa rafiki yake maeneo ya
Magomeni-Kagera jijini Dar es Salaam.
Mtandao huu unatoa pole kwa wanafamilia, ndugu, jamaa na marafiki wa marehemu Abdul Bonge kwa msiba huu uliotokea.
MUNGU AILAZE ROHO YA MAREHEMU ABDUL BONGE MAHALI PEMA PEPONI. AMEN.
(Picha zote na Dustan Shekidele, GPL, Morogoro)
USIPITWE! JIUNGE NASI FACEBOOK
TOA MAONI YAKO HAPA (MATUSI HAYARUHUSIWI)
Filed Under:
WASANII
on Tuesday, March 31, 2015
Note: Only a member of this blog may post a comment.