Thursday, February 19, 2015

Anonymous

Ustadhi aliyelawiti mwanafunzi wake aongezewa miaka 15 jela

Mwalimu wa madrasa ya Kadiria iliyopo Amani mjini Zanzibar, Hamad Bakar Mohammed, anayetumikia kifungo cha miaka 15 jela kwa kosa la kumlawiti mwanafunzi wake wa kiume, ameongezewa adhabu nyingine ya miaka 15 jela na Mahakama ya Rufaa Tanzania.

Hukumu hiyo ilikuja baada mshitakiwa huyo kupinga kifungo cha miaka 15 alichopewa na Mahakama Kuu Zanzibar baada ya upande wa mashtaka kupinga uamuzi wa mahakama ya Mkoa wa Vuga, kumuachia huru mshitakiwa.

Adhabu hiyo ilitolewa na Jaji wa Mahakama Kuu Zanzibar,Abdul- hakim Ameir Issa. 
Uamuzi wa kumuachia huru mshitakiwa huyo katika mahakama ya Vuga, ulitolewa na Hakimu Makame Mshamba Simgeni, baada ya kusema ushahidi uliotolewa na upande wa mashtaka hautoshi kumtia hatiani.

Jopo la majaji watatu akiwemo Jaji Kimano, Jaji Njasiri na Jaji Luonda, walitupilia mbali rufaa ya mshitakiwa kupinga kifungo hicho na badala yake ikaamua kumuongezea kifungo cha miaka 15.

Adhabu hiyo mpya sasa inamfanya mshitakiwa huyu kutumikia kiufungo cha miaka 30 jela.

Wakitoa hukumu, majaji hao walisema vitendo hivyo vimekithiri licha ya kukemewa na Serikali na kwamba adhabu hiyo itakuwa fundisho kwa wengine wenye tabia kama hiyo.

Hukumu hiyo ilitolewa Februari 13 mwaka huu huku upande wa mashtaka ukiwakilishwa na Maulid Ame Mohammed kutoka Ofisi ya Mkurugenzi wa Mashtaka.
FAIZA WA MHESHIMIWA SUGU: HAKUNA STAA MWENYE FIGA KAMA YANGU! 
===>>SOMA ZAIDI HAPA!
JIUNGE NASI FACEBOOK > >>BONYEZA HAPA.KAMA KUNA TATIZO AU UNA PICHA ZA MATUKIO TUTUMIE WHATSAPP +255 712 919 142. 
ASANTE NA KARIBU TENA!

USIPITWE! JIUNGE NASI FACEBOOK

Subscribe to this Blog via Email :

TOA MAONI YAKO HAPA (MATUSI HAYARUHUSIWI)

Note: Only a member of this blog may post a comment.