Mbongo-Fleva, Nasibu Abdul ‘Diamond Platnumz’ akiwa na mama yake Sanura Kassim.
MUSA MATEJA/AmaniHAKUNA neno linaloweza kusemwa kwa mara nyingine zaidi ya Mungu ni mwema! Kauli hiyo inakuja kwa mara nyingine baada ya mama mzazi wa Mbongo-Fleva, Nasibu Abdul ‘Diamond Platnumz’, Sanura Kassim a.k.a Sandra kurejea nchini akiwa yupo fiti.
Habari rasmi kutoka chanzo cha kuaminika zinaeleza kwamba, mama mzazi wa Diamond amerejea nchini wikiendi iliyopita huku hali yake ikionekana kuimarika vizuri tofauti na mwanzo ambapo alirejeshwa nchini akiwa hoi kufuatia kushambuliwa na ugonjwa wa kupooza mkono na mguu.
“Cha msingi anamshukuru Mungu kurejea kwa afya yake ambapo kwa sasa yupo fiti, kaondokana na tatizo la kupooza, kwa sasa anaweza kutembea na kushika chochote kwenye mkono.
Jirani wa mama huyo ambaye hakupenda jina lake kuandikwa alisema kitendo cha mama Diamond kurejea akiwa na afya njema kimemfurahisha sana.
INASIKITISHA SANA: MWANDISHI ALBINO AELEZEA ALIVYONUSURIKA KIFO MARA MBILI!
===>>SOMA ZAIDI HAPA!
JIUNGE NASI FACEBOOK > >>BONYEZA HAPA.KAMA KUNA TATIZO AU
UNA PICHA ZA MATUKIO TUTUMIE WHATSAPP +255 712 919 142.
===>>SOMA ZAIDI HAPA!
ASANTE NA KARIBU
TENA!


Note: Only a member of this blog may post a comment.