Mchungaji Mchungaji Josephat Gwajima
Nakala ya barua kutoka kwa Meneja wa Mkoa wa Kinondoni wa NHC.
KANISA la Mchungaji Josephat Gwajima lililokuwa
likiendesha shughuli katika viwanja vya Tanganyika Packers Kawe, wilaya
ya Kinondoni, jijinI Dar limeamriwa kuondoka eneo hilo.
Kanisa hilo ambalo kwa muda mrefu limekuwa likiendesha shughuli zake
eneo hilo limedaiwa kusababisha usumbufu na kero kubwa za makelele kwa
wakazi wa maeneo hayo.
Barua iliyosainiwa na Meneja wa Mkoa wa Kinondoni wa Shirika la
Nyumba la Taifa, B.N. Masika, imesisitiza kwamba pamoja na kutambuliwa
umuhimu wa kanisa hilo kuendesha shughuli zake shirika hilo
halitaweza kutoa ruhusa kwa kanisa hilo kuendelea kufanya mahubiri
katika viwanja hivyo,kwani shirika hilo limeshaanza kutumia viwanja
hivyo kwa maendeleo ya wananchi wa Kawe ikiwa ni ujenzi wa makazi n.k
Barua hiyo imetoa 30 zinazoishia tarehe 9 Machi mwaka huu ili Mchungaji Gwajima ajitayarishe kuondoka eneo hilo.

Note: Only a member of this blog may post a comment.