
Wabongo Fleva Juma Mussa ‘Jux’ na Vanessa Mdee ‘Vee Money’ wakila ujana.
Wawili hao walikutwa wamepakatana wakati wa onyesho la kutambulisha
video za wakali wa Bongo Fleva, lililofanyika mwishoni mwa wiki katika
viwanja vya Escape One, Mikocheni jijini Dar.
Juma Mussa ‘Jux’ akipozi.
Baada ya Vanessa kumaliza shoo yake, ukafuata wakati wa Jux ambaye
alipomaliza na kurudi nyuma ya jukwaa, Vee alimpisha mvulana huyo akae
kitini kisha yeye akamkalia, jambo lililotosha kuwaaminisha watu mapenzi
yao.“Njooni muone jamani Vanessa kapakatwa na Jux tena hawana hata wasiwasi wenyewe wamejiachia kama hawapo vile, watakuwa ni wapenzi tu kwa maana huwa wanaficha sana,” alisikika akisema shabiki.
Hawakuishia hapo, kwani waliendelea kuoneshana mahaba mpaka walipoondoka katika viwanja hivyo.
JIUNGE
NASI FACEBOOK > >>BONYEZA HAPA.KAMA KUNA TATIZO AU
UNA PICHA ZA MATUKIO TUTUMIE WHATSAPP +255 712 919 142.ASANTE NA KARIBU
TENA!
-RISASI Mchanganyiko


Note: Only a member of this blog may post a comment.