Thursday, February 12, 2015

Anonymous

Mauaji Ya Wanafunzi Watatu Waislamu Marekani Yazua Hisia Kali

Watu wa familia moja waliouawa huko Caroline Kazkazini.
Maafisa wa polisi mjini Carolina kazkazini nchini Marekani wamemkamata mtu mmoja baada ya wanafunzi watatu waislamu kupatikana wamefariki nyumbani mwao.

Miili ya Deah Barakat,mkewe Yusor Mohammed Abu salha na dadaake Razan Mohammed Abu salha ilipatikana siku ya jumanne ikiwa na majeraha ya risasi katika vichwa.

Mtu mmoja mwenye umri wa miaka 46 tayari amefunguliwa mashtaka kutokana na mauaji hayo.

Maafisa wa polisi wanasema wanajaribu kubaini iwapo mauaji hayo yanatokana na chuki.

Swala kwamba wanafunzi waliouawa ni waislamu limezua uvumi katika mitandao ya kijamii wa iwapo mauaji hayo ni ya kidini au la Uchunguzi uliofanywa umebaini kwamba uhalifu huo ulitekelezwa kutokana na mzozo unaondelea kuhusu uegeshaji wa magari,maafisa wa polisi wa Chapell. 
BIG SOO: Ommy Dimpoz Aambulia Matusi ni Baada ya Kupost Tangazo la CCM!
===>>SOMA ZAIDI HAPA!
JIUNGE NASI FACEBOOK > >>BONYEZA HAPA.KAMA KUNA TATIZO AU UNA PICHA ZA MATUKIO TUTUMIE WHATSAPP +255 712 919 142.ASANTE NA KARIBU TENA!

USIPITWE! JIUNGE NASI FACEBOOK

Subscribe to this Blog via Email :

TOA MAONI YAKO HAPA (MATUSI HAYARUHUSIWI)

Note: Only a member of this blog may post a comment.