Ishu hiyo iliyopata nafasi kwenye vyombo mbalimbali vya habari, ilitokana na Jide kuwapa watu nafasi mashabiki wake kumuuliza maswali katika mtandao wa kijamii, ambapo asilimia kubwa walitaka kujua kama kweli ameachana na mume wake au la.
Magazeti Pendwa kutoka Global Publishers yakaamua kumtafuta Gardner ili aweke bayana juu ya suala la ndoa yao kutokana na mwanamuziki huyo kuweka wazi kwamba tayari ndoa yao ilikwishasambaratika.
...Wakiwa kwenye pozi.
Siku chache zilizopita mwanamuziki Jide alifunguka kwamba hakutaka
tena kuendelea kuishi na mume wake kutokana na tabia mbaya alizokuwa
nazo mwanamume huyo, hali iliyomfanya kuishi pasipo kuwa na furaha
katika kipindi kirefu cha ndoa yao.Akifunguka zaidi, Jide alisema kwamba alichoshwa na tabia hizo ambazo alipobanwa zaidi ili aziweke wazi tabia hizo, alisema kwamba mwanamume huyo alikuwa na tabia ya kuwashikashika wanawake kila alipokuwa jukwaani akiimba.
Wawili hao walifunga ndoa Mei 14, 2005, jijini Dar es Salaam ambapo mpaka wanaachana, hawakubahatika kupata mtoto.
JIUNGE NASI FACEBOOK > >>BONYEZA HAPA.KAMA KUNA TATIZO AU
UNA PICHA ZA MATUKIO TUTUMIE WHATSAPP +255 712 919 142.
ASANTE NA KARIBU
TENA!


Note: Only a member of this blog may post a comment.