Chanzo cha kuaminika kutoka ndani ya Jeshi la Polisi mjini hapa, kimeiambia Kandili Yetu kuwa watu hao walikamatwa jana saa 5 asubuhi katika eneo la Kijiji cha Amboni Mafuriko, baada ya kuonekana katika eneo hilo wakiwa wanashangaa na hawajui wanakokwenda.
Baada ya kuonekana kwa watu hao, wananchi wa kijiji hicho kilicho jirani na Kijiji cha Mleni ambako kundi la wahalifu wa silaha lilijificha, walitoa taarifa kwa polisi ambao walifika na kuwatia mbaroni.
“Ni kweli leo (jana) saa tano asubuhi huku eneo la Kijiji cha Amboni Mafuriko kuna watu wawili wenye asili ya Somalia walikamatwa baada ya wananchi kuwaona na kuwatilia shaka, na hivyo kufanikisha kukamatwa,” kilisema chanzo hicho.
Wakizungumza na mwandishi wa habari hizi, ndugu wa watuhumiwa hao walidai ndugu zao wamekamatwa na polisi siku tatu zilizopita.
“Kuna ndugu zetu wawili wameshikiliwa kwa mahojiano kwa zaidi ya siku tatu na hatujawahi kuwaona kila tukiwapelekea chakula na dhamana imekataliwa, hivyo hali hiyo inatupa wasiwasi mkubwa,” alisema mmoja wa ndugu wa watuhumiwa hao ambaye hakutaka jina lake litajwe.
Mbali na matukio ya kukamatwa watu hao, hali ya ulinzi katika Hospitali ya Rufaa ya Bombo imeimarishwa, hasa katika wodi ambayo askari waliojeruhiwa kwenye tukio la Amboni wamelazwa wakiendelea na matibabu.
Kandili Yetu ilimpotafuta Kamanda wa Polisi Mkoa wa Tanga, Fraser Kashai pamoja na Kamishna Mkuu wa Operesheni na Mafunzo nchini, Paul Chagonja, wote walisema wapo katika kikao cha Kamati ya Ulinzi na Usalama.
BREAKING NEWS: [PICHAZ] BASI LA KIDIA ONE LAGONGANA USO KWA USO NA LORI DODOMA!
===>>SHUHUDIA HAPA!
JIUNGE NASI FACEBOOK > >>BONYEZA HAPA.KAMA KUNA TATIZO AU
UNA PICHA ZA MATUKIO TUTUMIE WHATSAPP +255 712 919 142.
===>>SHUHUDIA HAPA!
ASANTE NA KARIBU
TENA!


Note: Only a member of this blog may post a comment.