Thursday, February 19, 2015

Anonymous

HUU NDIO UKWELI: COMEDY NYINGI ZA KIBONGO ZINADHALILISHA WANAWAKE!

Mwigizaji wa kike wa filamu Ligth butterfly Mushi ‘Light’ amefunguka kwa kusema kuwa hapendi kuigiza Komedi kwa sababu ni udhalilishaji hasa kwa wanawake, anasema kuwa aliwahi kuchaguliwa kucheza Komedi ya Inye lakini baadae aligundua kilichofanya achaguliwe ni maumbile yake.

“Tunaigiza filamu hakuna udhalilishaji lakini kuna Komedi tuliwahi kucheza ilikuwa inataka wasanii wa kike wawe na maumbile makubwa yaani makalio, kuchesha makalio sasa huo si uchekeshaji ni udhalilishaji, hicho ndio kilinifanya nichukie Komedi,”anasema Light.

Light anasema kuwa waandaaji wasiangalie tu maslahi yao tu pia waangalie waigizaji nao maisha yao baadae wakiwa na familia zao na wakiangalia filamu zao za Komedi zilizotolewa siku za nyuma watakuwa katika hali gani, hali ambayo inamfanya asipende kuigiza Komedi.
JIUNGE NASI FACEBOOK > >>BONYEZA HAPA.KAMA KUNA TATIZO AU UNA PICHA ZA MATUKIO TUTUMIE WHATSAPP +255 712 919 142. 
ASANTE NA KARIBU TENA!

USIPITWE! JIUNGE NASI FACEBOOK

Subscribe to this Blog via Email :

TOA MAONI YAKO HAPA (MATUSI HAYARUHUSIWI)

Note: Only a member of this blog may post a comment.