Msanii wa filamu za Kibongo, Doreen Reguna ‘Queen Magali’
Richard Bukos/Mchanganyiko
MSANII wa filamu za Kibongo, Doreen Reguna ‘Queen Magali’ amefunguka kuwa kifo cha staa wa Bongo Fleva, Moses Mshagama ‘Mez B’ ni pigo kubwa sana kwake kwani marehemu alikuwa ni mpenzi wake na alikuwa na mimba yake.
MSANII wa filamu za Kibongo, Doreen Reguna ‘Queen Magali’ amefunguka kuwa kifo cha staa wa Bongo Fleva, Moses Mshagama ‘Mez B’ ni pigo kubwa sana kwake kwani marehemu alikuwa ni mpenzi wake na alikuwa na mimba yake.
Akizungumza na gazeti hili huku akionesha sura ya masikitiko, Queen
Magali alisema kinachomuuma zaidi ni kwamba, ujauzito wa marehemu
aliokuwa nao, ulichoropoka saa chache baada ya kupokea taarifa za msiba
huo.
“Nilipopigiwa simu kwa mara ya kwanza, sikuamini, hata ndugu zake
marehemu walinipigia simu, sikuamini hadi nilipompigia shangazi yake
ambaye alinithibitishia msiba huo, hapohapo nikapata mshutuko, hali
yangu ikawa mbaya hadi nikalazwa.
“Nashukuru Mungu kwa sasa naendelea vizuri.
“Kiukweli msiba huu
kwangu umekuwa ni pigo kubwa, tulikuwa na mipango mingi na marehemu
katika maisha yetu, alishanitambulisha kwa ndugu na jamaa zake wote wa
karibu lakini nasikitika zaidi kwa kuwa nimechelewa kuhudhuria mazishi
ya mpenzi wangu kutokana na kuzidiwa ghafla lakini nitafanya kila
liwezekanalo ili nikaweke japo mchanga kwenye kaburi la mtu niliyempenda
katika maisha yangu,” alisema Queen Magali.
Baadhi ya wapenda ‘ubuyu’ waliokuwa wakisikiliza mahojiano ya Queen
Magali na mwanahabari wetu, walisikika wakihoji kwa nini mrembo huyo
asianike uhusiano wake na Mez B kabla hajafariki lakini mwenyewe alidai
walikubaliana uchumba wao uwe wa siri.
Mez B alifariki dunia nyumbani kwao Dodoma Ijumaa iliyopita ambapo alizikwa katika makaburi ya Wahanga wa Reli, Dodoma.
JIUNGE NASI FACEBOOK > >>BONYEZA HAPA.KAMA KUNA TATIZO AU
UNA PICHA ZA MATUKIO TUTUMIE WHATSAPP +255 712 919 142.
ASANTE NA KARIBU
TENA!


Note: Only a member of this blog may post a comment.