Friday, February 27, 2015

Anonymous

MAAJABU MOROGORO: FAMILIA YALALA NJE KWA HOFU YA UCHAWI!

Dunstan Shekidele, Morogoro
NDUMBA? Katika hali isiyotarajiwa, familia tatu za Nasibu Salum ‘Mbunge’, mkazi wa Kitongoji cha Lukole Kijiji cha Fulwe, Kata ya Mikese wilayani Morogoro Vijijini, zimelazimika kuishi nje ya nyumba zao kwa zaidi ya siku tano kukwepa mauzauza yanayodaiwa kuwa ya kishirikina yaliyokuwa yakiwatokea. 

Tukio hilo la aina yake lilitokea hivi karibuni kijijini hapo ambapo awali, baba wa familia (Salum) alichapwa makofi na watu wasioonekana mbele ya mkewe na wanaye huku nyumba nyingine zikivamiwa na moto wa ajabu. 

Imeelezwa kuwa, wakiwa usingizini moto ulizuka kwa mpigo katika nyumba hizo tatu ambapo katika jitihada za kuokoa maisha yao ndipo walipoamua kutoa samani za ndani nje na wao kulala nje pia.

Mwanahabari wetu alifika eneo hilo na kushuhudia wanafamilia hao wakiwa nje ya nyumba hizo na mali zao. Alipoulizwa sababu za kutoa samani zao na kulala nje, Salum (pichani) alisema:
“Hizi ni fitina za majirani zangu, hawapendi maendeleo yangu, mauzauza haya yalianza tangu mwezi Desemba, mwaka jana nilipomalizia nyumba yangu ya tatu.“Wakati wa kuezeka nyumba hiyo nilimkabidhi mke wangu fedha shilingi milioni moja, nikamwambia mafundi wakimaliza kazi awakabidhi haki yao, cha ajabu kwenye fedha hizo laki mbili ziliyeyuka kimaajabu. 

“Siku iliyofuata mke wangu aliweka fedha ya michezo yao ya akinamama kwenye sidiria ili kuzipeleka sehemu husika, alipofika huko shilingi elfu 10 zilikuwa zimeyeyuka.”“Kama hiyo haitoshi nyumba zangu zote tatu hazina umeme lakini usiku moto wa ajabu unazuka na kuunguza nguo za mke wangu pekee na godoro tunalolalia na mke wangu limechorwa vitu vya ajabu. Ijumaa: Kuna mtu yeyote unamhisi kuhusika na tukio hili?

Salum: Kuna jirani yangu sitaki kumtaja ambaye ni mpinzani wangu kibiashara, nahisi anahusika.
Ijumaa: Kwa sasa una mpango gani wa kukabiliana na majanga haya?

Salum: Kama unavyoona muda huu amekuja mwenyekiti wa kitongoji, pia atakuja diwani wa kata ambapo tutakaa kikao kitakachotoa jibu.

USIPITWE! JIUNGE NASI FACEBOOK

Subscribe to this Blog via Email :

TOA MAONI YAKO HAPA (MATUSI HAYARUHUSIWI)

Note: Only a member of this blog may post a comment.