Friday, February 13, 2015

Anonymous

LIVE: Majibu ya Ommy Dimpoz kuhusiana na picha zilizoenea akiwa na Ex wa Diamond Platnumz

Miongoni mwa stori zilizochukua headline mitandaoni hata kwenye magazeti ni kuhusu picha ya hitmaker wa ‘Ndangushima’ Ommy Dimpoz akiwa na ex wa Diamond Platnumz ,Wema Sepetu kitandani wamelala pamoja na picha zingine zilizozua mjadala mkubwa. 

Sasa leo Feb 12 Ommy Dimpoz ame amplify kwenye Amplifaya ya Clouds FM na kusema ; ‘Ni picha tu mimi naona kama ni picha zingine tu za kawaida, sasa nimeshindwa kuelewa kwanini labda zimetengeneza sana stori kwasababu mimi naona sio mara yangu kwanza kupiga picha na Wema hata uki google utaona tunapicha nyingi sana kwa hiyo sijaelewa kwanini zimeleta stori.

May be nafikikiri zilizotengeneza stori zaidi ni hizi ambazo zinaonesha tuko chumbani kwasababu mimi nilikuwa nimelala kiukweli na tulikuwa tunakaa kwenye apartment moja nilikua nimeshtukia picha zipo kwenye mitandao unajua unavyokaa kwenye apartment kwasababu tulienda kwenye matembezi binafsi na washikaji wengine tulikua wengi wengi kidogo tulienda South Africa unajua mnavyokaa kama familia kunakuwa na mambo ya utani utani nimeshtukia tu picha zimeenea kwahiyo hata watu wakiniuliza ninawambia wamuuliza aliyepiga picha hizo
Millardayo ; “…Wengi wanafahamu kuwa wewe ni mshikaji wa Diamond Platnumz imekuaje sasa hivi kuonekana kwenye picha na Ex wa Diamond Platnumz,Wema Sepetu…?”

Ommy Dimpoz ; “…Sidhani kama kuna tatizo kwasababu hawa wote ni watu wangu nimefahamia nao siku nyingi nimekuwa nao karibu katika kipindi tofauti kabla hawajakuwa kwenye uhusiano mimi tayari ni watu wangu sidhani mimi nianze kuelezea sijui ooh nilikuwa labda na Wema sehemu, Wema ni mshikaji wangu tangia siku nyingi kwa hiyo hata kama alikuwa katika uhusiano na Diamond yakatokea mahusiano yao pengine hayapo sasa hivi hayawezi kunifanya mimi kuharibu ushikaji wangu kwasababu hivyo ni vitu vyao personal…“Alisema.
Unaweza uka bonyeza play kumsikiliza Ommy Dimpoz akihojiwa kwenye #Amplifaya Feb 12  
MATATIZO KATIKA UZALISHAJI WA MBEGU ZA KIUME (LOW SPERM COUNT) 
===>>SOMA ZAIDI HAPA!
JIUNGE NASI FACEBOOK > >>BONYEZA HAPA.KAMA KUNA TATIZO AU UNA PICHA ZA MATUKIO TUTUMIE WHATSAPP +255 712 919 142. 
ASANTE NA KARIBU TENA!
-millardayo   

USIPITWE! JIUNGE NASI FACEBOOK

Subscribe to this Blog via Email :

TOA MAONI YAKO HAPA (MATUSI HAYARUHUSIWI)

Note: Only a member of this blog may post a comment.