Dustan shekidele, Morogoro
MTOTO wa mhudumu wa baa aliyefia gesti hivi karibuni mjini hapa, Zaria Kambi aliyefahamika kwa jina la Rashid lsmail ameibua simanzi kufuatia kuachwa na mama yake wakati bado alikuwa akimhitaji kwa msaada wa kumtibu.
Taarifa zilizopatikana baada ya kifo cha Zaria zinaeleza kuwa, tatizo la mtoto huyo kuwa na uvimbe kwenye kitovu ndilo lililomsukuma mama yake atafute kazi baa.
“Inasikitisha sana, unajua Zaria (marehemu) alikwenda kutafuta kazi baa baada ya kukosa pesa ya kumtibu mwanaye. Sasa amefariki kabla ya kutimiza azma yake,” alieleza mmoja wa marafiki wa marehemu aliyeomba hifadhi ya jina lake.
Akizungumza na gazeti hili bibi wa mtoto huyo, Mwajuma Hassan alisema mjukuu wake huyo alikuwa na tatizo hilo tangu alipozaliwa na mwaka huu alitakiwa kufanyiwa upasuaji. “Kwa kweli ni masikitiko makubwa sana, mjukuu wangu huyu zilikuwa zinahitajika shilingi 1,200,000 ili afanyiwe upasuaji lakini hali imekuwa ngumu,” aliongea kwa masikitiko mama huyo.
Zaria ambaye inadaiwa ni dada wa msanii Selemani Msindi ‘Afande Sele’ hivi karibuni alikutwa ameuawa kikatili katika Gesti ya Stavi (Gesti ya Marafiki) iliyopo Kichangani, mjini Morogoro.
Yeyote aliyeguswa na tatizo la mtoto Rashidi awasiliane na mjomba wake aitwaye Ally Abdallah Kambi aliyepewa jukumu la kumlea kwa namba 0654233726.

Note: Only a member of this blog may post a comment.