Wednesday, February 11, 2015

Anonymous

Hivi unaweza kuacha CASH mezani kwako na ujumbe eti mwizi akiingia azichukue? Isome hii

Hakuna mtu anayependa uhalifu hata kidogo, lakini vipi unakutana na mtu ambaye anaacha pesa ndani ya nyumba yake pamoja na ujumbe kwa mwizi yoyote ikitokea kaingia ndani ya nyumba basi ajichukulie kiurahisi!

Nakusogezea kutoka China, wanandoa wameacha hela kwenye meza kiasi cha Yuan 300 (sawa na sh. elfu 85 Tshs) pamoja na ujumbe ambao unamtaarifu mwizi yoyote atakayeingia achukue hela hizo.

Imekuwa kawaida yao kufanya hivyo, safari hii walikuwa wakisafiri kwenda Shenzhen, Kusini mwa China safari ambayo walipanga kukaa kwa miezi miwili.
Ujumbe waliouacha unasomeka hivi; “Najua umehangaika sana mwaka huu. Lazima una hamu ya kuwaona wazazi wako, chukua pesa hizi kakate ticket ya treni na uende kuwasalimia. Kama ukirudi utafute kazi ya heshima“
 
Ujumbe wa wanandoa hao pamoja na cash waliyoiacha kwenye meza yao.
Mwaka 2010 waliwahi kusafiri na kuacha pesa na ujumbe kama huo, waliporudi walikuta mlango umevunjwa na pesa zimeibiwa lakini hakuna kitu chochote kingine ambacho kimeibiwa ndani ya nyumba yao.
JIUNGE NASI FACEBOOK > >>BONYEZA HAPA.KAMA KUNA TATIZO AU UNA PICHA ZA MATUKIO TUTUMIE WHATSAPP +255 712 919 142.ASANTE NA KARIBU TENA!
-millardayo

USIPITWE! JIUNGE NASI FACEBOOK

Subscribe to this Blog via Email :

TOA MAONI YAKO HAPA (MATUSI HAYARUHUSIWI)

Note: Only a member of this blog may post a comment.