
Bado kuna utata kuhusu kinaachoendelea juu ya afya ya Bobbi Kristina, mtoto wa pekee wa Marehemu Whitney Houston, mengi yanaendelea kuzungumzwa kuhusu hali yake huku wengine wakisema kuwa leo ni siku ambayo familia hiyo imeruhusu madaktari kumtoa mashine ya kupumulia ambayo aliwekewa toka siku ambayo alifikishwa hospitali baada ya kukutwa akiwa ameanguka ndani ya bafu, Georgia Marekani.
Baada ya yote kusikika familia ya Bobbi huyo
imeamua kutumia kampuni ya wanasheria wao kutoa maelezo rasmi kuhusu
kila ambacho kimesikika kuhusu hali ya mtoto huyo, taarifa hiyo
imekanusha uvumi wote uliowahi kusikika ikiwemo ishu ya kumtoa mipira ya
kupumulia siku ya leo ambapo ni siku ambayo mama yake alifariki.
Katika taarifa hiyo ya Wanasheria wa
familia hiyo wamesema wanaangalia namna ya kuwachukulia hatu wote
waliotoa taarifa za uongo ikiwemo waliosema walizungumza na wahusika wa
familia hiyo kitu ambacho sio kweli.
Marehemu Whitney Houston akiwa na mtoto wake Bobbi Kristine wakati akiwa mdogo.
TMZ, The National Enquirer, The Atlanta Journal Constitution na the Daily Mail ni sehemu ya vyombo vya habari ambavyo vimelaumiwa kwa kuandika taarifa za uongo.
Bobbi Kristina akiwa na Oprah Winfrey
Bado hakuna taarifa rasmi ambayo familia hiyo imetoa kuhusu hali ya mtoto huyo, leo inatimia miaka miaka mitatu tangu afariki Whitney Houston ambaye alikutwa pia.
PICHAZ: RAIS JK AFUNGUA JENGO LA NSSF LA KITEGA UCHUMI MOSHI!
===>>JIONEE HAPA!
JIUNGE
NASI FACEBOOK > >>BONYEZA HAPA.KAMA KUNA TATIZO AU
UNA PICHA ZA MATUKIO TUTUMIE WHATSAPP +255 712 919 142.ASANTE NA KARIBU
TENA!
PICHAZ: RAIS JK AFUNGUA JENGO LA NSSF LA KITEGA UCHUMI MOSHI!
===>>JIONEE HAPA!

Note: Only a member of this blog may post a comment.