Friday, February 27, 2015

Anonymous

HABARI+PICHAZ: Watu 3 wafariki dunia kwa kuungua moto hadi kuteketea kabisa akiwemo dereva na utingo wake.

Watu watatu wamefariki dunia kwa kuungua moto hadi kuteketea kabisa akiwemo dereva na utingo wake baada ya lori la mafuta kuacha njia na kupinduka na kuungua moto katika eneo la Maseyu barabara ya Morogoro-Dar es Salaam.
Kikosi cha zimamoto walichukua muda kuuzima moto huo kutokana na kusambaa ambapo hata hivyo hakukua na matukio ya watu kujitokeza kuiba mafuta kama ilivyozoeleka.

Baada ya kumaliza kuuzima moto huo kikosi cha zimamoto na uokoaji wakafanya juhudi nyingine za kuvuta kwa craine na kukata kwa kutumia mashoka mabaki ya lori hilo baada ya walioshuhudia tukio hilo kueleza kuwa watu wote waliokuwemo katika gari hawakutoka ambapo baada ya muda miili mitatu iliokolewa ikiwa imeungua kabisa.
Kwa mujibu wa mashuhuda wa tukio hilo wakiwemo madereva wa malori ambapo walikuwa wakisafirisha mafuta katika kampuni moja Farhan Yusufu amesema lori hilo lilikua limesheheni mafuta ya Dezel mali ya kampuni ya Petrol Africa ilikua ikitokea Dar es salaam kwenda jijini Mwanza ambapo ilipoteza uelekeo na kupinduka kisha kuwaka moto.

Waliofariki dunia ni Ahmed Dilie dereva na utingo wake aliyefahamika kwa majina ya Emela na mtu mmoja ambaye bado hajaweza kufahamika mara moja.
[PICHAZ+VIDEO] LAZIMA UKAE! Enjoy na hii ya zoezi la nguvu analopiga babu wa miaka 60..  
===>>JIONEE MWENYEWE HAPA! JIUNGE NASI FACEBOOK > >>BONYEZA HAPA.KAMA KUNA TATIZO AU UNA PICHA ZA MATUKIO TUTUMIE WHATSAPP +255 712 919 142. 
ASANTE NA KARIBU TENA! 
Chanzo: ITV

USIPITWE! JIUNGE NASI FACEBOOK

Subscribe to this Blog via Email :

TOA MAONI YAKO HAPA (MATUSI HAYARUHUSIWI)

Note: Only a member of this blog may post a comment.