Monday, February 23, 2015

Anonymous

Diamond Platnumz, Chege na ndugu wa marehemu Mez B wamesikika kwenye 255 leo, FEB23

Story ya kwanza kusikika kwenye 255 leo February ilikuwa inahusu kuvuja kwa wimbo wa Diamond na Iyanya ambapo baada ya kuvuja wimbo huo watu walihisi ni collabo ya Diamond na P Square.
Dia & Iyanya
Diamond amesema collabo hiyo imefanyika siku nyingi baada ya show ya Fiesta, ilifanywa kabla ya kufanyika wimbo wa ‘My Number One Rmx’ lakini imeachiwa wiki iliyopita baada ya kuonekana imevuja tayari mitandaoni.
Kulikuwa na mvutano kwenye social networks kuhusiana na kilichoandikwa na mtangazaji mmoja TZ ambapo aliweka picha ya Chege na wasanii wenzake kwenye ukurasa wake Instagram wakiwa wamevaa tshirt zilizoandikwa RIP Mez B pamoja na vitambaa vyeusi mkononi huku kukiwa na post iliyouliza kitambaa kile cheusi kama ni hirizi.
Chegge
Chege ameongea kwenye 255na kuonyeshwa kukasirishwa na kitendo hicho, alipotafutwa mtangazaji huyo amemuomba radhi Chege na kusema yeye alijua kabla hajaweka post hiyo kuwa ile sio hirizi ilikuwa ni kitambaa.
Ya mwisho kusikika ni kutoka Dodoma ambapo ndugu wa marehemu Mez B walitoa ratiba ya leo ambapo mazishi yatakuwa yakifanyika Dodoma.
Mez-B
Neema Steven ambaye aliwahi kusimamia project za mwisho za marehemu Mez B amesema alikuwa rafiki wa msanii huyo na walikuwa marafiki wa karibu zaidi baada ya msiba wa msanii Mangwea, mkataba wao uliisha baada ya mwaka mmoja na nusu lakini mpaka anafariki walikuwa kwenye mikakati ya kufanya kazi tena kwa pamoja.
JIUNGE NASI FACEBOOK > >>BONYEZA HAPA.KAMA KUNA TATIZO AU UNA PICHA ZA MATUKIO TUTUMIE WHATSAPP +255 712 919 142. 
ASANTE NA KARIBU TENA! 
-millardayo 

USIPITWE! JIUNGE NASI FACEBOOK

Subscribe to this Blog via Email :

TOA MAONI YAKO HAPA (MATUSI HAYARUHUSIWI)

Note: Only a member of this blog may post a comment.