Wachezaji wa Chelsea
Mkufunzi
wa timu ya Everton Robert Mertinez amewashtumu wachezaji wa Chelsea kwa
kujaribu kumshawishi refa katika mechi iliyotawaliwa na hasira nyingi
kutoka kwa wachezaji wote ambapo Chelsea ililazimika kufunga bao la
dakika za mwisho ili kuilaza Everton 1-0 uwanjani darajani.Bao la dakika za lala salama la Willian liliwekwa wavuni baada ya Gareth Barry kupewa kadi nyekundu huku ugomvi ukizuka baada ya Branislav Ivanovic kumchezea visivyo James McCarthy wa Everton tukio ambalo lilikwepa adhabu ya refa.
''Ni wazi kwamba kile wachezaji wa Chelsea walijaribu kufanya ni kumshawishi refa'',Martinez aliiambia BBC.
Mourinho alikatiza mahojiano yake na BBC wakati alipoulizwa kuhusu nidhamu ya wachezaji wa Chelsea.
Mechi iliokuwa iende sare iliimarika katika dakika za mwisho baada ya Gareth Barry kupewa kadi ya pili ya njano kwa kumuangusha Willian.
Huku wachezaji wa pande zote mbili wakikabiliana, Ivanovic alimkaba koo Mc Carthy na kuonekana akitaka kumpiga kichwa kiungo huyo wa kati wa Everton.
HAIJAWAHI KUTOKEA: Kijana wa miaka 17 apunguzwa uume baada ya kupitilza kiwango!
===>>SOMA ZAIDI HAPA!
JIUNGE
NASI FACEBOOK > >>BONYEZA HAPA.KAMA KUNA TATIZO AU
UNA PICHA ZA MATUKIO TUTUMIE WHATSAPP +255 712 919 142.ASANTE NA KARIBU
TENA!
===>>SOMA ZAIDI HAPA!
-BBC


Note: Only a member of this blog may post a comment.