Friday, December 23, 2016

Unknown

Paul Makonda Amtaka DC wa Ubungo Kufuata Nyayo Zake!

Mkuu wa Mkoa wa Dar es Salaam, Paul Makonda leo (Alhamisi) amemwapisha Mkuu mpya wa Wilaya ya Ubungo, Kisale Makori na kumtaka kutokaa ofisini na kusubiri taarifa badala yake atoke nje na kusikiliza kero za wananchi wa wilaya hiyo.

Makonda amesema changamoto kubwa ya watendaji ni uwajibaki na kwamba baadhi yao hupenda kusubiri kupelekewa taarifa za wananchi ofisini badala ya kuwafuata wananchi katika maeneo yao.
"Naomba Makori usiwe mtu wa kusubiri taarifa ofisini pekee.Wanaubungo wanamatumaini makubwa na wewe kwa sababu umeaminiwa na Rais (John Magufuli),"amesema Makonda.

USIPITWE! JIUNGE NASI FACEBOOK

Subscribe to this Blog via Email :

TOA MAONI YAKO HAPA (MATUSI HAYARUHUSIWI)

Note: Only a member of this blog may post a comment.