Thursday, December 22, 2016

Unknown

KRC Genk ya Samatta imepoteza mchezo dhidi ya Zulte-Waregem... Cheki Msimamo Hapa!

Ligi Kuu soka Ubelgiji iliendelea usiku wa December 21 2016 kwa michezo kadhaa kuchezwa, timu ya KRC Genk inayochezewa na mtanzania Mbwana Samatta ilikuwa mgeni wa timu ya Zulte-Waregem katika uwanja wa Regenboog. 
KRC Genk ikiwa ugenini imekubali kupoteza mchezo kwa goli 1-0, goli ambalo lilifungwa na  Souahilo Meite dakika ya 26 ya mchezo, kwa matokeo hayo KRC Genk wanakuwa na takwimu kwa mechi zao 5 zilizopita kushinda mechi 2, kufungwa mechi 2 na kutoka sare mchezo mmoja.  
Kwa upande wa Mbwana Samatta kocha wake Peter Maes ameendelea kumuamini na kumpanga kwa dakika zote 90, mchezo uliyopita Genk walilazimishwa sare ya kufungana goli 2-2 na Standard de Liege goli la pili la kusawazisha la Genk lilifungwa na Mbwana Samatta dakika ya 78.

USIPITWE! JIUNGE NASI FACEBOOK

Subscribe to this Blog via Email :

TOA MAONI YAKO HAPA (MATUSI HAYARUHUSIWI)

Note: Only a member of this blog may post a comment.