Wednesday, December 21, 2016

Unknown

IDADI YA WALIOFARIKI KWA KUNYWA SABUNI WAKIFIKIRI NI POMBE IMEFIKIA HIVI...

Idadi ya watu waliofariki baada ya kunywa sabuni wakidhania ni pombe imefikia watu 58 kutoka 49 kulingana na vyombo vya habari nchini Urusi, Wengi wa watu 37 walioathirika bado wanaendelea kutibiwa huku wengine wakiwa katika hali mahututi.

Raia hao walikunywa maji ya sabuni yaliokuwa na sumu kali wakidhania ilikuwa pombe kulingana na kamati ya uchunguzi ya Urusi,lakini maji hayo yalikuwa na kemikali ya Ethanol inayoweza kusababisha upofu.

USIPITWE! JIUNGE NASI FACEBOOK

Subscribe to this Blog via Email :

TOA MAONI YAKO HAPA (MATUSI HAYARUHUSIWI)

Note: Only a member of this blog may post a comment.