Saturday, December 17, 2016

Unknown

BREAKING News: Rais Magufuli Katengua Uteuzi wa Dr. Mwele Malecela

Taarifa kutoka IKULU inasema Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt. John Pombe Magufuli, tarehe 16 Desemba, 2016 ametengua uteuzi wa Mkurugenzi Mkuu wa Taasisi ya Taifa ya Utafiti wa Magonjwa ya Binadamu (NIMR) Dkt. Mwele Malecela.
Uteuzi wa Mkurugenzi Mkuu wa NIMR atakayejaza nafasi iliyoachwa wazi na Dkt. Mwele Malecela utatangazwa baadaye. 

December 15 2016 Dr. Mwele alinukuliwa na vyombo vya habari Tanzania akizungumza kuhusu uwepo wa ugonjwa wa ZIKA Tanzania na kwamba asilimia 15 ya waliopimwa walikutwa na virusi vya ugonjwa huo ambapo hata hivyo taarifa hizo zilikanushwa na wizara ya afya leo.

USIPITWE! JIUNGE NASI FACEBOOK

Subscribe to this Blog via Email :

TOA MAONI YAKO HAPA (MATUSI HAYARUHUSIWI)

Note: Only a member of this blog may post a comment.