Wednesday, December 21, 2016

Unknown

Arusha Kujenga Machinga Complex Yao

KATIKA kutekeleza agizo la Rais John Magufuli, uongozi wa Jiji la Arusha umeanza mchakato wa kujenga jengo la kufanyia shughuli za biashara wafanyabiashara wadogo maarufu ‘Wamachinga.’

Eneo lililotengwa kwa mradi huo lipo katikati ya Jiji, kwenye kiwanja Namba 69 chenye ukubwa wa zaidi ya ekari moja, sehemu ambayo ilirejeshwa serikalini na Waziri Mkuu, Kassim Majaliwa wakati wa ziara yake mkoani Arusha hivi karibuni.

Kiwanja hicho kilichopo mkabala na soko la Kilombero, linadaiwa awali liliuzwa kinyemela na madiwani wa halmashauri, kabla ya Waziri Mkuu kuamuru lirudishwe na tayari eneo hilo limerudi serikalini.

Akizungumzia hilo, Mkurugenzi wa Halmashauri ya Jiji la Arusha, Athumani Kihamia alisema eneo hilo lina uwezo wa kuhifadhi wafanyabiashara wadogo zaidi ya 2,000 pamoja na shughuli mradi utakapokamilika. Jiji la Arusha lina wakazi takribani 500,000.

Mmoja wa machinga anayeuza viatu, Hussein Issa, amesema hilo ni jambo jema, huku akushauri kusiwe na urasimu wakati wa ugawaji wa maeneo yaliyotengwa kwa ajili yao.

USIPITWE! JIUNGE NASI FACEBOOK

Subscribe to this Blog via Email :

TOA MAONI YAKO HAPA (MATUSI HAYARUHUSIWI)

Note: Only a member of this blog may post a comment.