UJUMBE ULIKUWAJE?
Katika ujumbe uliokuwa unasambaa, picha ya message ‘screen shot’ ya meseji iliyodaiwa kutoka kwa mama Diamond, ilikuwa ikionesha kwamba mwanamke huyo alikuwa akiomba msaada kwa shoga yake wa kumsaidia ‘kumchamba’ Zari mitandaoni na kama ikiwezekana, waende kumroga ili aachane na Diamond.
TEAM ZARI WATOKWA POVU
Baada ya kunaswa kwa ujumbe huo, kundi linalomsapoti Zari kwenye mitandao ‘Team Zari’ lilianza kumshambulia mama Diamond kwa kumshushia mitusi ya nguoni na kumtuhumu kwamba eti yeye ndiye amekuwa chanzo cha mwanaye kutodumu na wanawake kwenye mapenzi kwa sababu anamuingilia na kumgombanisha nao.

MAMA DIAMOND AJA JUU
Baada ya kusikilizia ‘machafuko’ yaliyokuwa yakiendelea kwenye mitandao ya kijamii, hasa Instagram, mwandishi wetu alimtafuta mama Diamond na kutaka kujiridhisha kama ujumbe uliokuwa ukisambaa mitandaoni ni kweli ulitoka kwake na sababu zilizomfanya aandike maneno hayo. Baada ya kumpata na kuzungumza naye, mama Diamond alikuja juu na kueleza kuwa ‘hapendagi ujinga’ linapokuja suala la mambo ya kifamilia, akakanusha kwamba ujumbe huo haukuwa umetoka kwake na kwamba ulitengenezwa na wabaya wake kwa lengo la kumchafulia sifa mbele ya jamii.
“Kwanza sipendagi ujinga mimi! Hata ukiangalia DP (display picture- picha ya utambulisho wa mtumiaji wa Instagram) haifanani na ninayotumia kwenye akaunti yangu halisi. Kwanza mimi ni mtu mzima na akili zangu, siwezi kutuma meseji kama hiyo, siwezi kuweka mambo ya kifamilia kwenye mitandao wala kwenye vyombo vya habari.
“Natukanwa sana mitandaoni hasa baada ya bethidei yangu na zaidi matusi yameongezeka baada ya mimi kum-wish hepi bethidei Wema (Sepetu- ex wa mwanaye) lakini sina muda wa kubishana nao, Mungu atawalipia,” alisema mama Diamond. Mwandishi wetu alipomuuliza ni hatua gani anafikiria kuwachukulia watu waliofanya mchezo huo, alisema awali alifikiria kwenda polisi lakini busara zikamtuma kuacha kwani akilipeleka suala hilo mbele ya sheria, watakaokamatwa ni wengi kwa sababu anatukanwa na wengi na haoni sababu ya kufanya hivyo.

Note: Only a member of this blog may post a comment.