Siku hizi nimekuwa nikiwaona baadhi ya akina Baba ambao binafsi nawaita wa ' hovyo hovyo ' wakija na Mabinti zao tena wakubwa tu Madukani na hasa katika Supermarkets mbalimbali na kuwanunulia ' Pedi ' tena kuna wakati unakuta ' Li Dingi ' hilo hilo bila hata chembe ya aibu linamchagulia ' Bintiye ' aina ya ' taulo ' za kutumia.
Najua humu kuna akina Mama zetu na Wazee wenye MAADILI kabisa hivi haya mambo ya ' hovyo hovyo ' wayafanyayo Wazazi wa siku hizi hasa wa Kiume kwa Mabinti zao hususan kuwanunulia ' Pedi ' na kujua kuwa wapo ' Moon ' wamerithi kwenu nikimaanisha kuwa na nyie huko nyuma mlikuwa mkifanyiwa hivi au ni ' Uzungu ' tu umetuharibu na tunakosa maadili na kujua mipaka ya Baba juu ya Binti yake ambaye ni mkubwa na ameshavunja Ungo?
Badilikeni Wanaume wenzangu na akina Baba na jifunzeni kujua mipaka yenu hasa kwa Mabinti zenu.
Asubuhi na Jumanne njema nyote.
Note: Only a member of this blog may post a comment.