Thursday, October 20, 2016

Unknown

Hivi Ndivyo Lionel Messi Alivyoinyanyasa Man City ya Pep Guardiola Nou Camp

Michuano ya Ligi ya Mabingwa Ulaya imeendelea tena usiku wa October 19 2016 kwa michezo nane tena kuchezwa kama iliyochezwa usiku wa October 18, mchezo wa Man City dhidi ya FC Barcelona katika dimba la Nou Camp ulikuwa ndio mchezo ulioteteka hisia za mashabiki wengi.
Mvuto wa mchezo huo ambao ulimalizika kwa mshindi wa tuzo ya mchezaji bora wa dunia mara 5 Lionel Messi kufunga hat-trick, ulikuwa unazikutanisha FC Barcelona dhidi ya kocha wao wa zamani Pep Guardiola mbaye kwa sasa ndio anaifundisha Man City.
Mchezo ulimalizika kwa FC Barcelona kuibuka na ushindi wa goli 4-0, licha ya kuwa mashabiki wengi wa soka walitarajia kuona Man City ikiisumbua FC Barcelona kutokana na Pep Guardiola kuwafahamu, kitu ambacho hakikuisaidia Man City, magoli ya FC Barcelona yalifungwa na Lionel Messi dakika ya 17, 61, 69 na Neymar dakika ya 89 baada ya kukosa penati dakika ya 87.
Matokeo mengine haya hapa: 

USIPITWE! JIUNGE NASI FACEBOOK

Subscribe to this Blog via Email :

TOA MAONI YAKO HAPA (MATUSI HAYARUHUSIWI)

Note: Only a member of this blog may post a comment.