Tuesday, September 13, 2016

Unknown

RAYMOND: Nilitamani Kuwaona WEMA na SNURA Kwenye Video ya ‘Natafuta Kiki’

Msanii wa WCB, Raymond amesema asingependa video ya wimbo wake ‘Natafuta Kiki’ itoke bila kuwepo kwa Snura na Wema Sepetu.

Akiongea na E! News ya EATV, Ray alisema wakati anashoot video hiyo, Wema Sepetu alikuwa busy hivyo ikambidi achukue moja ya clip ambazo walishoot wakiwa pamoja kwenye birthday party ya Romy Jons.

Raymond na Snura
“Mimi sina ugomvi na Wema ndio maana hata nilipomwona kwenye party ya Romy Jons nikaenda kumsalimia na camera men wakachukua video,na mwanzoni nilishaongea naye kuhusu yeye kutokea kwenye video ya Natafuta kiki lakini ratiba zake zikabana,” alisema.
“Na mimi nilishasema moyoni mwangu natamani niwaone Snura na Wema kwenye Natafuta Kiki,kwahiyo nikawa sina jinsi,” aliongeza Ray.

USIPITWE! JIUNGE NASI FACEBOOK

Subscribe to this Blog via Email :

TOA MAONI YAKO HAPA (MATUSI HAYARUHUSIWI)

Note: Only a member of this blog may post a comment.