Thursday, September 22, 2016

Unknown

Mkasa: Kijana atorokwa na mke wake siku chache baada ya kufika Dar na kuachiwa mtoto wa miezi 9 Tu

Kijana mmoja ambaye jina lake halikupatikana mara moja ameachwa solemba na mke siku chache baada ya kufika Dar es salaam wakitokea Bukoba.
Kijana aliyetorokwa na mke wake akiwa na mwanae wa miezi 9.
Kijana huyo na mke wake pamoja na mtoto wao wa miezi 9 walifika Dar es salaam kwa jili ya kutafuta maisha.

Baada ya kufika Dar es salaam walikaa gesti kwa siku kadhaa, na baadae waliamua kutafuta chumba, na baada ya chumba kupatikana kwa msaada wa dalali, kijana alimwambia mkewe akatoe hela kwenye simu ili walipie chumba lakini mwanadada huyo alitoroka moja kwa moja na kumuachia mume wake mtoto mdogo wa miezi tisa.

Baada ya kuhangaika sana kumtafuta mkewe ambaye amemuachia mtoto mdogo wa miezi tisa, aliamua kwenda Clouds FM kutangaza na baadaye mtangazaji wa kipindi cha Leo Tena, Dahuu waliweza kumsaidia kijana huyo kwa kumpeleka mtoto kwenye dawati la jinsia.

Lakini Ijumaa hii, yule mwanamke baada ya kusikia matangazo kwamba amepotea, aliamua kumtumia ujumbe huu mume wake “Umenitangaza mimi nimepotea lakini mimi sijapotea nipo na hela zote nimetoa nimeenda kufanya yangu, nilikuwa nasubiria mtoto akuwe. Kwa hiyo watoto nimekuachia uwalee ila hata siku moja usije ukathubutu kuoa, mimi ni mke wako na nitarudi muda wowote. Nashukuru kwa upendo wako najua unaipenda sana, kwa hiyo nimeondoka mwenyewe wala haujanikosea chochote na nitarudi mwenyewe. Nakutakia kila la kheri,”.

Ujumbe wa mwanamke huyo
Je una maoni gani kwa kijana huyo?

USIPITWE! JIUNGE NASI FACEBOOK

Subscribe to this Blog via Email :

TOA MAONI YAKO HAPA (MATUSI HAYARUHUSIWI)

Note: Only a member of this blog may post a comment.