Meneja anayewasimamia wasanii wa WCB wakiwemo Harmonize na Raymond, Ricardo Momo, amekanusha tetesi kuwa mafahari hao wamekuwa wakivimbiana na kwamba kila mmoja anajiona bora.
“Hayo ni maneno tu, sisi tunaishi kama ni familia moja, natamani siku moja uje uone tunavyoishi, tunataniana , tupo kwenye shida tunasaidizana,” amesema.
“Hakuna hata mmoja mwenye ugomvi na mwenzake, hayo ni maneno tu ya watu wa nje, hakuna matatizo yoyote yaliyotokea kati ya Harmonize na Raymond.”
Note: Only a member of this blog may post a comment.