Thursday, September 15, 2016

Unknown

Hatimaye Mama WEMA Amalizana na Man Fongo... Pia Afunguka Kuhusu Kujiunga INSTAGRAM

Ukitaja story ambazo zimekiki kinoma noma wiki iliyopita huwezi kuacha kuitaja ile ya Mama Wema Sepetu na King wa Singeli Man Fongo. Mengi yalizungumzwa na pia hata wahusika kusikika kulizungumzia hilo lakini mwisho wa siku utu uzima dawa. Mama Wema ameamua kufunguka kuwa hana tatizo na Man Fongo.Ni pale Mama Wema alipofuatwa nyumbani kwake na Nafia Afrika na kufanyiwa interview baada ya sakata hilo kupamba moto. 

Ndipo Mama Wema alifunguka “Ninachotaka kusema ni kwamba, mimi natamka wazi sina tatizo na yule mtoto” Mama Wema alifunguka kwamba katika vitu ambavyo hawezi kuvifanya, kimoja wapo ni kujiunga katika mtandao wa Instagram. Alidai kwamba akijiunga katika mtandao huo atakwazika na mengi, bali yeye mtandao ambao anaufurahia kuutumia ni Whatsapp.

USIPITWE! JIUNGE NASI FACEBOOK

Subscribe to this Blog via Email :

TOA MAONI YAKO HAPA (MATUSI HAYARUHUSIWI)

Note: Only a member of this blog may post a comment.