Thursday, September 1, 2016

Unknown

LUPITA Nyong’o Aanza Misele na Mpenzi Wake Mpya Raia wa Nigeria

Lupita akiwa na mpenzi wake Mobolaji Dawodu
Lupita Nyong’o ameonekana kwa mara ya kwanza akiwa na mpenzi wake mpya mwanamitindo mwenye asili ya Nigeria, Mobolaji Dawodu.

Siku chache zilizopita ziliibuka tetesi za wawili hao kuwa na mahusiano lakini Jumanne hii wameonekana kwa mara ya kwanza wakiwa pamoja kwenye mchezo wa tennis kwenye mashindano ya US Open huko jijini New York wakati Serena Williams alipokuwa akicheza na Ekaterina Kakarova.

Siku chache zilizopita Lupita alithibitisha kuwa na mahusiano na mwanamitindo huyo huku akidai kuwa amemua kumweka mahusiano yake mitandaoni baada ya kumchunguza kwa muda wa miezi sita.
Dawodu ni mwanamitindo lakini pia ni muhariri wa jarida la mitindo GQ la nchini Marekani.

USIPITWE! JIUNGE NASI FACEBOOK

Subscribe to this Blog via Email :

TOA MAONI YAKO HAPA (MATUSI HAYARUHUSIWI)

Note: Only a member of this blog may post a comment.